Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kuwa mashaka ya mamilioni ya watu duniani yanachochewa na migogoro zaidi ya 120 ambayo inaendelea bila kusita.
Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa ametoa kipaumbele kwa hali ya Sudan na Ukraine ambapo watu karibu milioni saba wamekuwa wakimbizi.
Amesema, raia hao hawatarejea katika makazi yao kama hawatakuwa salama kwa muda mfupi na kwa muda mrefu bila ya kusitishwa machafuko.
Wakati huo huo, Grandi amesema "ingawa UNHCR si sehemu ya oparesheni ya Umoja wa Mataifa huko Gaza, hali ya raia katika eneo hilo ambayo tulidhani haiwezi kuwa mbaya zaidi, inafikia viwango vipya vya kukata tamaa kila siku. Siwaelezi wajumbe wa baraza hili jambo ambalo hamlijui bali huu ndio ukweli wa ulimwengu wetu," amesema Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa UN.
Grandi pia amekosoa suala la siasa kuwa na nafasi kuu duniani katika kukwamisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwa walioathiriwa na mizozo na vita.
342/
Your Comment