1 Mei 2025 - 23:35
Source: Parstoday
Ismail Baqaei: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimegonga mwamba

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uraibu wa Marekani wa kuwekea vikwazo mataifa mengine na kubainisha kwamba, vikwazo vya Washington dhidi ya Tehran vimeshindwa na kutokuwa na natija.

Ismail Baqaei ametahadharisha juu ya madhara ya mienendo ya Marekani inayokinzana na misimamo ya kichochezi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya watu binafsi na vyombo vya kisheria vya Iran na nchi nyingine kadhaa kwa kisingizio cha kushirikiana na Iran katika nyuga mbalimbali za kiuchumi na kibiashara.

Sambamba na kuashiria siasa za uadui, haramu na zisizo za kibinadamu za Marekani dhidi ya taifa la Iran, Baqaei amevichukulia vikwazo vya kikatili vya nchi hiyo dhidi ya Iran kuwa ni ukiukaji wa misingi na kanuni za kimsingi za sheria za kimataifa zikiwemo viwango vya haki za binadamu.

Ismail Baqaei: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimegonga mwamba

Aidha ameeeleza kuwa, vikwazo hivyo ambavyo vimetangazwa siku chache zilizopita dhidi ya shakhsia na makampuni ya Iran na yasiyo ya Iran kwa visingizio mbalimbali ni ishara tosha ya sisitizo la watunga sera wa Marekani la kuvunja sheria na kukiuka haki na maslahi ya nchi zingine, pamoja na juhudi zao za kuvuruga uhusiano wa kirafiki na kisheria kati ya nchi zinazoendelea kupitia ugaidi wa kiuchumi.

Vile vile amevitaja vikwazo hivyo ambavyo vinatekelezwa kwa mujibu wa sera iliyofeli na ya jinai ya mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya taifa kubwa la Iran kama ushahidi mwingine wa wazi wa mitazamo inayokinzana ya wafanya maamuzi wa Marekani na ukosefu wao wa nia njema na umakini katika kuendeleza njia ya diplomasia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha