10 Mei 2025 - 22:03
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu atoa wito kwa dunia nzima kupinga uhalifu wa Israel na Marekani huko Gaza

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameutaka Ulimwengu wa Kiislamu kutoruhusu suala la Palestina lisahaulike akisisitiza ulazima wa kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo Jumamosi akihutubia kundi kubwa la wafanyakazi kutoka kote nchini katika mji mkuu, Tehran.

"Sera za upendeleo ambazo zinatekelezwa ulimwenguni hii leo dhidi ya mataifa mbalimbali zinalenga kufanya masuala yanayohusiana na Palestina yasahaulike; mataifa ya Kiislamu hayapaswi kuruhusu jambo hili; hayapaswi kuruhusu hili lifanyike," amesema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

"Kupitia uvumi wa aina mbalimbali, kauli za aina tofauti, na kwa kuibua masuala mapya yasiyo na maana, wanajaribu kuondoa akili za watu kwenye suala la Palestina. Fikra za umma hazipaswi kuondolewa kwenye suala la Palestina," amesisitiza Ayatullah Khamenei.

Ameashiria uungaji mkono wa pande zote wa Wamagharibi kwa Israel katika ukatili wake huko Gaza na kuitaka jamii ya kimataifa kusimama kidete na kukabiliana na utawala huo ghasibu na waungaji mkono wake.

Amesema, jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza, Palestina, sio jambo linaweza kupuuzwa. Ulimwengu wote lazima usimame dhidi yake.

Kiongozi Muadhamu atoa wito kwa dunia nzima kupinga uhalifu wa Israel na Marekani huko Gaza

Imam Ali Khamenei amesisitiza kwamba: Walimwengu wanapaswa kusimame dhidi ya utawala wa Kizayuni wenyewe, na wanapaswa kukabiliana na  waungaji mkono wa utawala huo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesisitiza kuwa Marekani na washirika wake kama vile Uingereza wanashiriki katika ukandamizaji wa utawala wa Israel dhidi ya watu wa Palestina hususan huko Gaza, na licha ya matamshi ya hadharani ambayo yanaweza kuonekana kuwa muhimu, mataifa hayo yanaisaidia kikamilifu Israel.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: "Ukweli wa mambo ni kwamba taifa linalodhulumiwa la Palestina, watu wanaodhulumiwa wa Gaza, leo hii sio tu wanakabiliana na utawala wa Kizayuni, lakini pia wanakabiliana na Marekani na Uingereza."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha