12 Mei 2025 - 22:25
Source: Parstoday
Wazayuni wahamaki baada ya Trump kukiri Wayemen ni mashujaa

Menashe Amir, mkurugenzi wa Redio ya Kizayuni ya Kol Yisrael ameshindwa kuficha hamaki zake kufuatia uamuzi wa hivi karibuni ya Trump na kusema: "Waisraeli wameshtuka kwamba leo Wahouthi nchini Yemen wamekuwa mashujaa!"

Amesema hayo katika mahojiano maalumu ya televisheni na kuonesha wazi jinsi alivyohamaki baada ya Trump kufikia makubaliano ya kusitisha vita na Yemen bila ya kuzuia mashambulizi dhidi ya maeneo ya Wazayuni.

Wakati huo huo Wazayuni wamehamakishwa na hatua ya Trump ya kufanya mazungumzo na HAMAS kuhusu kuachiliwa huru mateka Mmarekani-Muisraeli bila ya kuishirikisha serikali ya utawala wa Kizayuni.

Kufuatia kutangazwa makubaliano kati ya Marekani na Hamas ya kumwachilia huru mfungwa wa Kizayuni mwenye uraia wa Marekani, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa baraza la mawaziri la Netanyahu halikushirikishwa hata kidogo kwenye mazungumzo hayo.

Kanali ya 12 ya Televisheni ya Israel imenukuu duru moja ya Kizayuni ikifichua kwamba, baraza la mawaziri la Netanyahu halikuwa na taarifa kuhusu mazungumzo ya Marekani na Hamas na limepokea tu ishara katika siku za hivi karibuni zinazoonesha kuwa, "Edan Alexander," mateka Mzayuni mwenye uraia wa Marekani amekaribia kuachiliwa huru.

Kanali ya 12 ya Israel imeongeza kuwa, kwa makubaliano hayo ya moja kwa moja na ambayo hayajawahi kushuhudiwa kati ya Hamas na serikali ya Marekani, Trump si tu amemzaba kibao Netanyahu, bali pia ameipa Hamas uhalali na ushindi usio na kifani tangu kuanza vita vya Oktoba 7, 2023.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha