14 Mei 2025 - 21:00
Source: Parstoday
Qalibaf: Umoja wa Mabunge ya Asia ni fursa ya kuendeleza uhusiano na nchi za Kiislamu

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia umuhimu wa Umoja wa Mabunge ya Kiislamu kwa ajili ya kustawisha uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na kusema: Kushiriki nchi 38 za Kiislamu katika mkutano wa 19 wa Mabunge ya Kiislamu ni fursa ya kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo.

Muhammad Bagher Qalibaf alisema jana usiku katika uwanja wa ndege wa Mehr- Abad mjini Tehran kabla ya kuelekea Jakarta kwa lengo la kushiriki katika Mkutano wa 19 wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) kwamba: Tunaelekea Jakarta kwa lengo la kushiriki katika Mkutano wa 19 wa PUIC; na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mabunge na mwenyeji wa Sekretarieti ya Muungano huu, ni mojawapo ya nchi wanachama wenye ushawishi mkubwa wa umoja huo. 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, zaidi ya jumbe 38 kutoka nchi za Kiislamu zinashirki katika mkutano huo na kwamba mkutano huo ni fursa nzuri ya kufanyika mazungumzo ya pande mbili kati ya nchi za Kiislamu kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano zaidi na kukabiliana na changamoto mbalimbali, hasa kadhia ya Palestina na Ukanda wa Gaza ambazo si tu ni masuala yanayouhusu Ulimwengu wa Kiislamu, bali ni daghadagha ya watu wote wapenda haki na wapigania uhuru duniani. 

Mkutano wa 19 wa Wabunge wa Umoja wa Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) unafanyika mjini Jakarta kuanzia Mei 12 hadi 15 chini ya mada "Utawala Bora na Taasisi Imara kama Nguzo za Ustahimilivu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha