Shirika la habari la habari la ABNA linaripoti kuwa: Bunge la Iraq leo limempa waziri mkuu Haidar al Abadi muda wa hadi siku ya alhamisi kuunda serikali mpya inayolenga kupambana na ufisadi imetangaza televisheni ya nchi hiyo.Waziri mkuu al Abadi alitangaza zaidi ya wiki sita zilizopita kwamba atachukua hatua ya kuitangaza serikali mpya itakayojumuisha wasomi ambao hawana maingiliano na kundi lolote la kisiasa. Kiongozi wa kidini mwenye usemi kutoka kundi la waislamu Shia lenye idadi kubwa nchini Iraq, Sayid Moqtada al Sadri aliongeza shinikizo dhidi ya waziri mkuu huyo hapo jana kwa kuanzisha hatua ya kulikalia eneo la usalama mjini Baghadad ambalo lina ofisi za kibalozi na serikali baada ya wafuasi wake kukita kambi kwenye eneo hilo zaidi ya wiki moja iliyopita.
Mwisho wa habari/ 291