23 Agosti 2016 - 18:59
Alqayarah yakombolewa nchini Iraq

Majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuzikomboa visima sita vya mafuta viliopo kusini mwa wilaya ya Musol baada ya mapambano makali yaliotokea leo hii kati ya majeshi ya Iraq na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo kwa kuikomboa sehemu hiyo ndio amekata njia ya mawasiliano baina ya magaidi wa Musol na sehemu zingine

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda wa mashambulizi ya kuikomboa wilaya ya Musol ametangaza kuwa: majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuikomboa sehemu ya Alqayarah baada ya mashambulizi makali yaliofanywa na majeshi ya anga ya Iraq na kusambaratisha sehemu muhimu ziliokuwa zimekusudiwa.
Majeshi ya Iraq pamoja nakuikomboa sehemu hiyo, pia wamefanikiwa kuvikomboa visima sita vya mafuta viliopo kusini mwa wilaya ya Musol na kuwasambaratisha magaidi waliokuwa waliviteka visima hivyo.
Msemaji wa taasisi ya kupambana na magaidi nchini Iraq amesema: sehemu ya Alqayarah mpaka sasa iko mikononi mwa majeshi ya Iraq, pia katika mapambano ya kuikomoa sehemu hiyo magari mengi ya kijeshi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh yameangamizwa.
Aidha “Raidu Amin Sheikhani” mmoja kati ya wanajeshi wa jeshi la Iraq amebainisha kuwa: jeshi la Iraq limefanikiwa kukata mawasiliano ya kikundi cha kigaidi cha Daeshi kiliopo Musol na waliopo katika sehemu nyingine kwa kuikomboa sehemu ya Alqayarah na visima sita vya mafuta ambapo sehemu hiyo ndio ilikuwa njia pekee ya mawasiliano yao na Daesh waliopo sehemu nyingine nchini Iraq.
Naye ameongeza kusema kuwa: hivi sasa kunapigano makali kati ya majeshi ya Iraq na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo majeshi ya anga ya Iraq nayo yanawasaidia majeshi ya chini katika mashambulizi hayo.    
mwisho wa Habari/290