Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Safa la Palestina, likinukuu vyanzo vya Kiebrania, kikosi maalum cha makomandoo wa jeshi la Israel kilivamiwa Ijumaa asubuhi katika eneo hilo, na kusababisha askari watano kuangamizwa papo hapo na wengine kadhaa wamejeruhiwa na hali yao ni mahututi. Makomandoo hao Waisraeli waliuawa na kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa jengo lililokuwa limetegwa kwa mabomu.
Shirika hilo liliongeza kuwa helikopta za kijeshi za Israel zilionekana zikifanya operesheni za uokoaji kwa kasi kubwa, zikiingia Gaza kuwasafirisha waliojeruhiwa.
Taarifa za zinasema vikosi maalum vya Israel vilikuwa vinaingia kukagua jengo na punde si pundi mlipuko mkubwa ulitokea na jengo liliwaporomokea wanajeshi 12 wa kikosi maalumu cha jeshi katili la Israel. Shughuli ya kuwaondoa kwenye kifusi ilikumbwa na ugumu mkubwa kutokana na makali ya mapigano yaliyoibuka.
Wakati huo huo, Brigedi za al-Qassam , tawi la kijeshi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas , limetangaza kufanikisha operesheni ya aina yake ya kijeshi dhidi ya majeshi ya Israel katika mji wa Jabalia, kaskazini mwa Gaza. Wamesema waliyalenga magari ya kijeshi ya Israel na kusababisha vifo na majeraha miongoni mwa askari wa kivamizi.
Al-Qassam imesema imeangamiza kifaru cha jeshi la Israel aina ya tiger kwa kutumia kombora la Yasin 105 pamoja na kifaa cha mlipuko cha Shawaz, Katika operesheni hiyo wanajeshi kadhaa wa Isarel wameuawa au kujeruhiwa.
Israel ilianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, baada ya vikosi vya Hamas kufanya operesheni ya kijeshi dhidi ya utawala huo wa Kizayuni kama jibu kwa ukatili uliokuwa umeongezeka dhidi ya Wapalestina.
Hadi sasa, utawala katili wa Israel umeshaua angalau Wapalestina 54,677 — wengi wao wakiwa wanawake na watoto , na kuwajeruhi wengine 125,530 katika Ukanda huo wa Gaza.
Katika uvamizi wake wa kikatili, Israel imelenga miundombinu ya raia, ikiwemo hospitali na shule, kwa njia inayokiuka wazi sheria za kimataifa.
Mwezi Novemba uliopita, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, pamoja na waziri wake wa zamani wa vita, Yoav Gallant, kwa mashitaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.
Pia, Israel inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutokana na uhalifu wake dhidi ya raia wa Palestina katika eneo hilo.
Your Comment