Maadhimisho haya yameandamana na swala za Idi katika misikiti na viwanja vya wazi, kuchinjwa kwa mifugo kama vile kondoo, ng’ombe au mbuzi kwa mujibu wa mila ya Kiislamu, na kugawa nyama kwa masikini na wahitaji kama alama ya mshikamano na ukarimu. Baadhi ya Waislamu pia wataadhimisha Sikukuu ya Idul Adh'ha kesho Jumamosi.
Sikukuu ya Idul Adh'ha huadhimishwa kila mwaka tarehe 10 ya mwezi wa Dhu al-Hijjah katika kalenda ya Kiislamu.
Sikukuu hii ni ukumbusho wa utiifu na imani ya Nabii Ibrahim (AS) kwa Mwenyezi Mungu, aliyeonesha utayari wa kumtoa mwanaye, Nabii Ismail (AS), kama dhabihu. Katika kilele cha imani hiyo, Mwenyezi Mungu aliteremsha kondoo kuchinjwa badala ya mwanaye.
Idul Adh'ha pia huashiria kilele cha ibada ya Hija ambayo hufanyika kila mwaka katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa Mamlaka Kuu ya Takwimu ya Saudi Arabia, mwaka huu jumla ya Mahujaji 1,673,230 wameitekeleza ibada hiyo, wakiwemo 1,506,576 kutoka nje ya nchi na 166,654 kutoka ndani ya Saudi Arabia.
342/
Your Comment