Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina ameonya kuhusu hali mbaya ya watoto katika Ukanda wa Gaza na kusema: "Kwa mujibu wa takwimu za awali, zaidi ya watoto 40,000 wameachwa yatima wakati wa vita, na idadi hii inaongezeka kwa kutisha."
Kadhim Abu Khalaf ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari kwamba tangu Oktoba 7, 2023, wastani wa watoto 27 wamepoteza maisha kila siku huko Gaza, takwimu isiyo na mfano ambayo hailinganishwi popote duniani.
Ripoti zinaeleza kuwa, idIdadi ya watoto wa Kipalestina walioachwa yatima kutokana vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza imepindukia 40,000, huku takriban wanawake 14,000 wakibakia wajane baada ya waume zao kuuawa kufuatia hujuma na mashambulio ya kinyama ya Israel katika ukanda huo
Msemaji huyo wa UNICEF pia ameashiria athari za kisaikolojia na kiakili za mzozo huo kwa watoto na kuongeza: "Watoto wa Gaza wanahitaji miaka ya kupona, sio tu kutokana na majeraha ya kimwili, lakini pia kutokana na kiwewe kikubwa cha kihisia na madhara ya kisaikolojia waliyoyapata."
Hapo awali Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) lilisisitiza katika taarifa yake kwamba watoto wa Gaza sio tu wanakabiliwa na kifo kutokana na shambulio mashambulio ya mabomu, bali pia maisha yao yanakabiliwa na kifo kutokana na njaa, ukosefu wa huduma za matibabu, na kuenea kwa magonjwa kutokana na ukosefu wa maji ya kunywa, na kwa upande mwingine, misaada ya kibinadamu kwa eneo hilo haiwezekani.
342/
Your Comment