Netanyahu ametoa ombi hilo ndani ya saa 48 zilizopita, kwa nia ya kuichochea Marekani kuingia moja kwa moja vitani baada ya Iran kutoa majibu makali yanayoifanya Israel ijute kuanzisha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Katika upande mwingine, Shirika la Habari la FARS limemnukuu waziri mkuu wa zamani wa Israel akiashiria kutokuwa na uwezo Tel Aviv wa kukabiliana na Tehran peke yake na kusisitiza kuwa, Israel haina uwezo wa kupigana vita na Iran peke yake kwa lengo la kuiangusha Jamhuri ya Kiislamu.
Kukiri huo Ehud Barak kumekuja baada ya majibu makali yaliyotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujibu uvamizi wa kigaidi uliofanywa na Israel katika ardhi ya Iran Ijumaa asubuhi. Amesema Israel haina nguvu za kuanzisha vita peke yake kwa lengo kuuangusha utawala wa Iran.
Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Israel amedai kuwa eti Israel ilipata mafanikio mengi baada ya kuua raia na maafisa wa kijeshi wa Iran siku ya Ijumaa lakini wakati huo huo amekiri uhakika mchungu kwao kwa kusema: "Sasa tunakabiliwa na changamoto ngumu na ndefu na tunaelekea kwenye mtihani mrefu na chungu."
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (SEPAH) usiku wa kuamkia leo limefanya wimbi jipya la mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya utawala wa Kizayuni, baada ya juzi kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa jina la "Ahadi ya Kweli III." Vyombo vya habari duniani vimetangaza kwamba mashambulizi ya jana ya Iran dhidi ya yalikuwa makubwa zaidi kuliko ya juzi Ijumaa.
342/
Your Comment