Leo Jumamosi, shirika la habari la IRNA limenukuu duru za habari za Kizayuni zikitangaza kuwa, meya wa mji wa Rishon Letzion ulioko kusini mwa Tel Aviv alisema jana Ijumaa kwa njia ya video kwamba: "Hii ni siku ngumu na yenye uchungu sana kwetu. Nilikuwa nimeona vitu vingi sana lakini sijawahi kuona uharibifu mkubwa kama huuu; matukio haya yanauma sana."
Licha ya kwamba utawala wa Kizayuni unachuja mno habari na unamtia mbaroni mtu yeyote anayepiga picha athari za mashambulizi ya Iran, lakini pamoja na hayo jana Israel ilikiri kwamba katika siku ya kwanza ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran, Wazayuni 80 wameangamizwa na kujeruhiwa huku hali ya baadhi ya majeruhi ikiwa mbaya sana.
Jana usiku vyombo vya habari vya Kizayuni viliripoti kuanza wimbi la tano la mashambulizi ya makombora ya Iran na kutangaza kuwa, wimbi la tano la makombora ya Iran limepiga maeneo yote ya Israel.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, wimbi la tano la makombora ya Iran limepiga maeneo ya Tiberias, Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na Galilaya ya Chini. Ving'ora vya tahadhari vilisikika katika maeneo hayo vikifuatiwa na sauti za miripuko mikubwa. Vyombo vya habari vya Kizayuni vilitangaza kuwa kutokana na udhibiti mkali, picha za vipigo vya makombora ya Iran kwenye maeneo hayo ni marufuku kuchapishwa na kusambazwa.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa, wakati wimbi la nne la makombora ya Iran limepiga maeneo ya kaskazini mwa Israel, wimbi la tano la makombora hayo limepiga maeneo yote ya Israel hata yale ambayo hayajawahi kushambuliwa, tena kwa usahihi mkubwa.
342/
Your Comment