15 Juni 2025 - 13:27
Source: Parstoday
HAMAS: Shambulio la Israel dhidi ya Iran ni kosa la kimkakati

Msemaji wa Brigedi za Al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya Hamas ametangaza mshikamano wake na Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na mashambulizi ya jana Ijumaa ya utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, Abu Obeida amesema hayo na kusisitiza kuwa, Hamas itaendelea kushikamana na Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.

Msemaji wa Brigedi ya Al-Qassam ameongeza kuwa: "Tunatangaza mshikamano wetu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya uchokozi wa kikatili wa utawala wa Kizayuni; uchokozi ambao umefanywa kwa makusudi kwa sababu ya misimamo imara ya Iran na uungaji mkono wake mkubwa kwa taifa na wanamapambano shupavu wa Palestina."

Abu Obeida pia ametoa mkono wa pole kwa kuuawa shahidi makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia wa Iran kwenye jinai hiyo ya Israel.

Msemaji huyo wa Brigedi za Al-Qassam ameeleza kuwa utawala huo ghasibu uko mwishoni tena mwa ghilba zake na unakosea mno kudhani kuwa jinai hizo zinaweza kudhoofisha misimamo ya kambi ya Muqawama au kuimarisha misingi dhaifu na tete ya utawala huo katika eneo.

Amesema: utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya makosa ya kimkakati na ya kihistoria kwa kufanya mashambulizi kama hayo na unazidi kujipeleka karibu na kuangamia kwake kikamilifu ambapo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kusambaratika Israel hakuepukiki.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha