Wanafunzi hawa, wapenzi wa Imam Hussein (as) na Hazrat Zainab (sa), wanaendelea kuonyesha kwa vitendo Nafasi ya Wanawake katika kuhifadhi utamaduni wa Kiislamu katika Mwezi huu Mtukufu wa Muharram; kupitia kushiriki kwao kikamilifu katika marasimu zote za Mwezi wa Muharram, na kuadhimisha kwa vitendo Mapinduzi ya Imam Hussein (as), kunako jumuisha uhuishaji wa maadili na misingi ya Kiislamu, ukumbusho wa dhabihu za Karbala, na msisitizo juu ya masomo na mafunzo yaliyomo ndani ya Mapinduzi hayo Matukufu ya Imam Hussein (as).
Hii ni pamoja na kufanya mikusanyiko kama hii ya Maombolezo, kuhuisha Marasimu ya A'shura, na kusisitiza umuhimu wa kufanya mageuzi, mabadiliko, kutetea haki na uadilifu, mambo ambayo Imam Hussein (as) aliyatolewa wito na kuyapa umuhimu mkubwa.
Your Comment