5 Agosti 2025 - 13:18
Wananchi wa Lebanon Wamiminika Mitaani Kumuunga Mkono Hizbullah na Muqawama

Wananchi waliokusanyika walisisitiza kuwa Hizbullah siyo tu ni ngome ya kijeshi, bali pia ni sehemu muhimu ya ulinzi wa taifa la Lebanon mbele ya vitisho vya mara kwa mara kutoka Israel, na kuvuliwa silaha kwao ni sawa na kuiacha nchi wazi kwa uvamizi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Wananchi wa Lebanon wametoka kwa wingi mitaani mjini Beirut kuonesha mshikamano wao na Harakati ya Hizbullah, kufuatia kuongezeka kwa shinikizo la ndani na nje ya nchi linalolenga kulazimisha harakati hiyo kuvuliwa silaha.

Wananchi wa Lebanon Wamiminika Mitaani Kumuunga Mkono Hizbullah na Muqawama

Waandamanaji hao walijitokeza usiku wa kuamkia leo katika mitaa ya eneo la Dahiyah ya Kusini mwa Beirut, wakiwa wamebeba bendera za Hizbullah na picha za viongozi wa harakati hiyo, huku wakipaza sauti kutetea “haki halali ya Muqawama (Mapambano) dhidi ya uvamizi wa kigeni.”

Mjadala kuhusu kuvuliwa silaha kwa Hizbullah umeibuka tena ndani ya duru za kisiasa nchini Lebanon na pia katika mazungumzo ya kidiplomasia, jambo ambalo wananchi wengi wa Lebanon wanalitazama kama njama ya Kizayuni inayolenga kuudhoofisha msimamo wa kitaifa wa nchi hiyo dhidi ya uvamizi wa Israel.

Wananchi waliokusanyika walisisitiza kuwa Hizbullah siyo tu ni ngome ya kijeshi, bali pia ni sehemu muhimu ya ulinzi wa taifa la Lebanon mbele ya vitisho vya mara kwa mara kutoka Israel, na kuvuliwa silaha kwao ni sawa na kuiacha nchi wazi kwa uvamizi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha