5 Agosti 2025 - 21:08
Maelfu waandamana Beirut kuunga mkono Hizbullah dhidi ya shinikizo la kuondolewa silaha

Wakisambaza ujumbe wao kwa sauti na maandamano, wananchi hao wamesisitiza kuwa Hizbullah si tu harakati ya kijeshi, bali pia ni nguzo muhimu ya taifa katika ulinzi wa mipaka na heshima ya Lebanon. Kwao, wazo la kuondoa silaha za harakati hiyo ni sawa na kuiweka Lebanon mikononi mwa maadui wake.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa Mnasaba wa Siku ya Thelathini tangu kuadhimishwa tukio la Karbala na kifo cha Bibi Sukaina binti Imam Husayn (a.s), Hauzatu Imam Ali (a.s) chini ya Bilal Muslim Mission Tanga, iliandaa Majlisi maalumu ya maombolezo katika Mji wa Pangani.
 
Katika hotuba hiyo, Sheikh Murtadha Khamisi alisisitiza kuwa: Uislamu umesimama juu ya msingi wa mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake (a.s), hivyo ni wajibu wetu kuendeleza majaalisi mbali mbali ili kuyahifadhi na kuyasimulia matukio haya kwa vizazi vyote.
 
Majlisi hizi ni fursa ya kuelezea historia ya mashujaa wa Karbala, hususan madhila ya Bibi Sukaina (a.s), ambaye alikufa shahidi akiwa bado mtoto kutokana na dhulma ya maadui wa Ahlul-Bayt(as).
 
Aidha, ilisisitizwa kuwa kuyaenzi matukio haya ya kihistoria si ibada tu, bali ni njia ya kufikisha ujumbe safi wa Uislamu kwa Waislamu na wasio Waislamu.
 
Kitengo cha Ripoti za Tabligh cha Hauza hiyo kimetoa mkono wa rambi rambi kwa waumini wote, kikieleza kuwa Mwenyezi Mungu awalipe wote wanaojitokeza na kuenzi misiba hii mitukufu, kwa malipo mema hapa duniani na akhera.
  
Maombolezo haya ni mwendelezo wa harakati za kuihifadhi roho ya Karbala na dhumuni la Imamu Husayn (a.s) la kurekebisha jamii kupitia elimu, sadaka ya nafsi, na kujitoa kwa ajili ya haki.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha