25 Oktoba 2025 - 17:26
Kurudi kwa Tishio la ISIS nchini Syria / Mashambulizi ya Kigaidi Yasambaa Raqa na Hasaka

Licha ya kupoteza udhibiti wa ardhi, kundi la ISIS bado lina uwezo wa kufanya mashambulizi ya milipuko, uvamizi wa ghafla na mauaji ya kulenga watu binafsi katika maeneo ya Raqa na Hasaka.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, mwaka 2025 umeona ongezeko kubwa la operesheni na mashambulizi yaliyofanywa na seli zilizobaki za ISIS katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya SDF (Syrian Democratic Forces) nchini Syria.

Shughuli hizi zimekuwa dhahiri zaidi katika Raqa na Hasaka, ambako mashambulizi ya ISIS yamekuwa yakitokea mara kwa mara - jambo linaloonyesha kuwa kundi hilo bado lina uwezo wa kusogea kwa siri na kutumia udhaifu wowote wa kiusalama kujijenga upya na kufanya mashambulizi ya ghafla.

Ingawa zaidi ya miaka saba imepita tangu ISIS kupoteza udhibiti wa ardhi katika maeneo hayo, bado ina uwezo wa kijeshi na kiusalama unaoiwezesha kufanya mashambulizi madogo madogo yanayotishia utulivu wa eneo hilo.

Mbinu za mashambulizi ya ISIS zimekuwa tofauti, zikiwemo milipuko, uvamizi wa kushtukiza na mauaji ya kulenga watu (assassination). Hali hii inathibitisha kuwa ISIS haijashindwa kabisa, bali inaendelea kujitahidi kubaki hai na yenye ushawishi katika uwanja wa usalama wa Syria.

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uangalizi wa Haki za Binadamu nchini Syria (Syrian Observatory for Human Rights), seli za ISIS zimefanya operesheni 31 katika maeneo ya Raqa na Hasaka tangu mwanzo wa mwaka 2025 hadi sasa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha