Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA kupitia mtandao wa Al-Mayadeen, vyanzo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimesema kuna hofu kwamba Rais wa Marekani Donald Trump ataweka shinikizo la kuanza hatua ya pili ya makubaliano ya Gaza bila Hamas kupokonywa silaha.
Kulingana na ripoti hiyo, Shirika la Utangazaji la utawala wa Kizayuni likinukuu vyanzo vyake limeongeza kuwa: "Makadirio yanaonyesha kuwa hatua ya pili ya makubaliano itaanza baada ya mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Trump." Pia, vyanzo hivyo vimeidai kuwa hatua ya pili ya makubaliano ya Gaza haitaanza kabla ya kurejeshwa kwa mwili wa mfungwa wa mwisho.
Your Comment