Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa, akisisitiza kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na migawanyiko ya ndani havina mshindi.

Akizungumza katika salamu zake za Sikukuu ya Krismasi, Waziri Mkuu amesema kuwa vita yoyote inayohusisha wananchi wa taifa moja husababisha hasara kwa pande zote bila mshindi, huku mgawanyiko wa kijamii na kisiasa ukiwa na matokeo ya kushindwa kwa taifa zima.
“Amani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa, lakini kupotea kwa amani kunaleta madhara yasiyokuwa na mshindi,” amesema Dr. Mwigulu Nchemba.

Waziri Mkuu amehitimisha kwa kuwatakia Wakristo wote nchini Tanzania heri ya Sikukuu ya Krismasi, huku akiwahimiza Watanzania wote, bila kujali tofauti zao za kidini au kijamii, kushikamana katika kujenga taifa lenye umoja, mshikamano na ustawi wa pamoja.
Your Comment