Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Sheikh Muhammad Hasan Jafari, Imam wa Ijumaa wa Skardu nchini Pakistan, alikutana na Ayatollah Sistani Mkuu, Kiongozi na Marjii wa juu wa Mashia, katika Mji wa Najaf Ashraf na kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala ya kielimu na kidini.
Katika mwanzo wa mkutano huu, Ayatollah Sistani (aliomba) dua kwa ajili ya Waumini wote wa Pakistan, hasa Waumini wa Gilgit-Baltistan, na kusisitiza kuwa Mashia wa Pakistan wanapaswa kuishi kwa umoja na mshikamano, na kupitia maadili, tabia, na matendo yao ya kila siku, waonyeshe taswira halisi ya Uislamu Halisi wa Mtume Muhammad (sawww) unaofuatwa na Madhehebu ya Shia Ithna Ashari.
Aidha, Ayatollah Sistani alikadiria sana huduma za kidini, kielimu na kijamii za Sheikh Muhammad Hasan Jafari.
Katika mkutano huo, mtoto wa Sheikh Muhammad Hasan Jafari pia alihudhuria.
Your Comment