
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- hafla hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka matabaka ya kidini na kijamii, waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
Sheikh Muhammad Niang alifariki dunia alfajiri ya Jumatatu, tarehe 8 Januari 2026. Alikuwa miongoni mwa wanazuoni mashuhuri na mhubiri mwenye juhudi kubwa, akihudumu katika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo nafasi ya Katibu wa Baraza la Wanazuoni wa Ahlul-Bayt (a.s) nchini Senegal.
Marehemu alitoa mchango mkubwa katika kueneza Uislamu wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s) na katika kuwatetea na kuwaunga mkono wafuasi wa madhehebu hayo nchini Senegal.

Mwenyezi Mungu amrehemu na amjaalie pahala pema peponi.
Your Comment