5 Februari 2026 - 11:07
Kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kushiriki katika mauaji ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah

Mwandishi wa habari wa Lebanon ametangaza kuwa mtu aliyeko chini ya ulinzi wa Idara ya Usalama wa Umma ya Lebanon alihusika kwa kushirikiana na Israel na kukusanya taarifa zilizopelekea kuuawa kwa Sayyid Hassan Nasrallah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- mwandishi wa Lebanon Abdullah Qamh amefichua kuwa mmoja wa waliokamatwa na vyombo vya usalama vya Lebanon ana mkono katika kesi ya mauaji ya Sayyid Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah.

Qamh alisema katika mahojiano ya televisheni:
“Mtu aliyeko kizuizini katika Idara ya Usalama wa Umma ya Lebanon, kwa mujibu wa uchunguzi, alishirikiana kwa njia isiyo ya moja kwa moja na utawala wa Kizayuni na hakuwa mwanachama wa Hizbullah. Amekiri mambo muhimu na hatari sana. Miongoni mwa kauli zake ni kwamba alikuwa akienda mara kwa mara katika eneo la Dahiya Kusini mwa Beirut akiwa na kundi la watu, na alikuwa na kifaa kidogo ambacho alikitumia kwenda maeneo maalumu ambayo baadaye ilibainika kuwa ni midomo ya mahandaki ya Hizbullah.”

Aliongeza:
“Kifaa hicho kilikuwa na uwezo wa kupima umbali kati ya uso wa ardhi na miundombinu ya chini ya ardhi, jambo lililosaidia Waisraeli kubaini aina na nguvu ya mabomu waliyohitaji kwa mashambulizi ya anga na kulenga kwa usahihi miundo hiyo.”
Qamh aliendelea kusisitiza kuwa, kwa mujibu wa maungamo ya mtu huyo, moja ya maeneo aliyoyatembelea ni eneo ambalo Sayyid Hassan Nasrallah alipata shahada.

Kwa mujibu wa taarifa, utawala wa Kizayuni tarehe 27 Septemba 2024 ulifanya operesheni ya kumuua Sayyid Hassan Nasrallah. Operesheni hiyo ilifanywa baada ya Israel kupata taarifa kuhusu kufanyika kwa kikao cha makamanda wa Hizbullah katika makao makuu ya harakati hiyo huko Dahiya Kusini mwa Beirut.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa ndege za kivita aina ya F-35 za utawala wa Kizayuni zilitumia mabomu mazito yanayopenya yenye uzito wa zaidi ya pauni elfu mbili, yaliyosababisha kubomolewa kabisa kwa majengo sita na kulengwa kwa makao ya Hizbullah.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha