29 Mei 2026 - 15:40
“Kwa Dhambi Gani Aliuliwa?” – Shahida Zahra Golpayegani Agusa Nyoyo za Wengi

Sheikh Muhammad Golpayegani, Mkuu wa Ofisi ya Imam Khamenei, amezungumzia kwa huzuni kuhusu shahida mdogo zaidi wa familia ya Imam Khamenei, mtoto Zahra Golpayegani, huku Aya za Surat At-Takwir zikikumbusha maumivu ya watoto wasiokuwa na hatia wanaouawa kwa dhulma.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Muhammad Golpayegani, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu Imam Khamenei (RA), ameelezea kwa huzuni kuhusu shahidi mdogo zaidi miongoni mwa mashahidi wa familia ya Imam Khamenei, akimzungumzia mtoto Shahida Zahra Golpayegani.

Katika maelezo hayo yaliyoambatana na Aya za Qur’ani Tukufu kutoka Surat At-Takwir, Sheikh Golpayegani alikumbusha kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
Na mtoto wa kike aliyezikwa hai atakapoulizwa: Kwa dhambi gani aliuliwa?” (At-Takwir: 8–9).

Shahida Zahra Golpayegani, ambaye alikuwa mjukuu wa Sheikh Muhammad Golpayegani na pia mjukuu wa Imam Khamenei, ametajwa kuwa miongoni mwa wahanga wasio na hatia waliopoteza maisha yao katika mazingira ya huzuni na majonzi makubwa.

Kauli hiyo imeibua hisia kali miongoni mwa wananchi na wafuasi mbalimbali, huku wengi wakitafakari juu ya thamani ya maisha ya watoto wasio na hatia na dhulma wanazokumbana nazo katika migogoro na mashambulizi mbalimbali duniani.

Kisa cha mtoto huyo shahida kimeendelea kugusa nyoyo za wengi, kikionekana kuwa mfano wa maumivu ya watoto wasiokuwa na kosa wanaopoteza maisha katika mazingira ya ukatili na dhulma.

Your Comment

You are replying to: .
captcha