Mamia kadhaa walijeruhiwa wakati mashapiki waliuvamia uwanja baada ya mechi kati ya timu mbili zinazoongoza kwenye ligi al-Masry na al-Ahly.
Mikutano ya dharura ya baraza la mawaziri pamoja na bunge imeitishwa.
Maandamano yamepangiwa kufanyika Alhamisi kulaani hatua ya polisi kutochukua hatua yoyote kuzima fujo hizo.
Mechi zote za ligi kuu nchini Misri zimeahirishwa kwa muda usiojulikana.
Mmoja wa mashabiki wa klabu ya al-Ahly ameiambia vyombo nya habari kwamba mashabiki wenzake wataandamana kutoka makao makuu ya klabu hiyo mjini Cairo hadi katika afisi za wizara ya mambo ya ndani.