24 Julai 2012 - 19:30

ABNA inatuarifu kuwa: Rais wa Ghana John Atta Mills amefariki wakati alipokuwa akipata matibabu.Wananchi na wakazi wa Ghana, wameanza maombelezi mara tu baada ya taarifa za kufariki kwake.

Hayati rais John Atta Mills 68 ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Ghana kwa kumshinda mpinzani wake Nana Akufo-Addo kwa kiasi kidogo cha kura mwaka 2008. Kufuatia kifo cha rais Attap-Mill, makamu wake wa urais John Dramani Mahama ameapishwa kuwa rais wa Ghana kuanzia sasa mpaka hapo uchaguzi wa rais mpya utakapo anza mwisho wa mwaka huu.