Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Kupamba moto habari za mwisho wa dunia katika tarehe 21 December 2012 za sababisha wengi kujiuliza maswali Je! Tarehe 21 December 2012 ndio mwisho wa dunia au ni propaganda na madai ya watu tu? Je! Madai ya mwisho wa dunia tarehe 21 December 2012 yanauhakika gani?.
Chimbuko la Madai ya mwisho wa dunia ni ndoto na utabiri wa kabila ya Maya ambapo walieleza kua tarehe 21 December 2012 ndio mwisho wa dunia kulingana na kalenda yao.
Kulingana na madai haya watu wengi waishi kwa hofu kutokana na habari hii kufikia baadhi yao kutengeneza Safina ya uokovu kunako janga hilo lilanozungumziwa kila siku hasa kukaribia tarehe hiyo.
Nchini Rusia watu zaidi ya Milioni mbili wameelekea katika handaki la mita 50 chini ardhi ambalo lilikuwa ni hifadhi ya jeshi la Umoja wa Sovyeti(Komonisti), Handaki hilo lilijengwa kwa lengo la kuhifadhi Wananchi kutokana na mabomu ya Nyuklia, Handaki hilo linaweza kustahamili bomu la Nyuklia lililotumiwa Hiroshima Japan na zaidi ya hilo.
Kulingana na nguvu na uwezo ulokua nao handaki hilo, Warusia walikimbia huko ili kujihifadhi na janga hilo, La ajabi ni kwamba pesa za tiketi za kuingia katika handaki hilo ni dola 1000.
Aidha kastazini mwa Ufaransa watu hawana amani kutokana na habari hiyo huku wakielezwa kua sehemu ya kwanza itakayo angamia ni kaskazini mwa nchi hiyo, Na hiyo ili sababisha wakazi wengi kuancha makazi yao kwa hofu ya siku hiyo.
Madai ya kuangamia ardhi na kua mwisho wake katika tarehe 21 December 2012 si sahihi kwa Dini zote zaitakidi kua kabla ya kuangamizwa dunia au kabla ya mwisho wa dunia lazima adhihiri muokozi wa watu kama Nabii Issa Ibn Mariam(as) na Imam Mahdi(as).
Aidha hakuna anaejua siku hiyo isipokua Mwenyezi Mungu pekee, Suala la kuangamia ardhi limeshazungumziwa katika Qurani Tukufu na kueleza jinsi itakavyo angamizwa ardhi na kila kilichomo ndani yake, Miongoni mwa ishara hizo za Qurani ni kama Aya ya 8 ya Surat Al-Rum, Aya ya Tatu ya Surat Al-Haqaf na Aya ya 48 ya Surat Ibrahim.
Kabla ya kuangamizwa ardhi itatokea zilzala kubwa sana kama ilivyoelezea Sura Zilzala, Mwanzo wake inaeleza kua itakapo karibia siku ya kiama itatetemeshwa ardhi mtetemesho na kutowa kila kilichomo ndani yake, Baada ya hapo ardhi itakua haina mmeya wa aina yoyote ile kiasi ya kwamba hata ukimleta yoyote kuishi hawezi kuishi aidha haya ni maneno ya Qurani Tukufu Surat Al-Kahf Aya ya 8.
Kwa mantiki hii ni kwamba kungamia dunia au kuwepo mweisho wa dunia hakuna shaka ndani yake ila kuangamizwa au kuangamia ardhi bila kudhihiri muokozi haiwezekani kutokana na imani na itikadi ya Dini na Vitabu kama Injili, Taurati, Zaburi na Qurani.
Nadharia na mtazamo wa Vitabu hiyo ni kua kamwe haiwezekani kuangamizwa au kuangamia ardhi kabla ya kudhihiri waokovu, Hiyo ni hadi ya Mwenyezi Mungu kuokowa watu kabla ya siku hiyo ya kiyama, Na madai ya kua tarehe 21 December 2012 ndio mwisho wa dunia sio kweli na haina uhakika ndani yake yote hayo ni propaganda na madai yasokua na ushahidi wowote ule.