9 Julai 2025 - 01:54

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Katika Masira ya Tasu'a Kwa ajili ya Kuomboleza Shahada ya Imam Hussein (as), Samahat Sheikh Ramadhan Kwezi, ameongea na Umma kupitia Televisheni ya IBN TV akibainisha kwamba Imam Hussein (as) ametufundisha na anatufundisha kuwa na Msimamo thabiti unaompendeza Mwenyezi Mungu (swt), alisisitiza kwamba tusikubali kamwe mtu yeyote aweze kuharibu jambo la Allah (swt). Akifafanua nukta hiyo amesema: Amani ni jambo la Allah (SWT), hivyo tuwe na Msimamo thabiti katika kuilinda amani yetu, na tusikubali mtu yeyote aharibu Amani na Utulivu tuliokuwa nao.

Your Comment

You are replying to: .
captcha