8 Julai 2025 - 15:25
Madrasat Hazrat Zainab(as) Kigamboni: Katika mwendelezo wa Maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein(a.s)  | "Baada ya Shahada ya Imam Hussein(as)" +Picha

Wasimamizi wa Programu hii: Wanafunzi Mabinti wa Hawza ya Hazrat Zainab (sa).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii - (Jana Jumatatu) - Tarehe 07 / 07 /2025 (inayosaidifiana na tarehe 11 Muharram 1447Hijiria), Majlisi kwa ajili ya Maombolezo ya Imam Hussein (a.s) imeendelea katika Madrasa ya Mabinti wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (s.a) - Kigamboni, Dar-es-Salaam - Tanzania,  ikihusiana na: "Baada ya Shahada ya Imam Hussein (as)".

Madrasat Hazrat Zainab(as) Kigamboni: Katika mwendelezo wa Maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein(a.s)  | "Baada ya Shahada ya Imam Hussein(as)" +Picha

Ufafanuzi zaidi kuhusiana na Majlisi hii:
Hii ni hafla ya maombolezo iliyopangwa kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kusikitisha ya Shahada ya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake waliouawa kishahidi katika jangwa la Karbala. Mada kuu ya kongamano hili iliangazia matukio na athari zilizofuatia baada ya Shahada ya Imamu Hussein(as). Hii inajumuisha:

1- Hatima ya familia yake na wafuasi wake waliobakia baada ya Shahada yake: Jinsi walivyoshughulikia msiba na matatizo waliyokumbana nayo baada ya vita hivyo vya Karabala.
2- Ujumbe na mafundisho yaliyoachwa: Jinsi harakati ya Imamu Hussein (as) ilivyoendelea kuhamasisha na kuathiri jamii na historia kwa ujumla.
3- Umuhimu wa Karbala: Maana na athari za Kisiasa, Kiroho, na kimaadili za tukio la Karbala kwa Waislamu, hasa Wafuasi wa Ahlul-Bayt(as).

Madrasat Hazrat Zainab(as) Kigamboni: Katika mwendelezo wa Maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein(a.s)  | "Baada ya Shahada ya Imam Hussein(as)" +Picha

Washiriki na Mgawanyo wa Majukumu:
Khutba ya Majlisi: Imetolewa na Mwanafunzi wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa), aitwaye: Na'imi Ayub. Khutba hii imetoa uchambuzi wa kina wa mada iliyotajwa hapo juu.

Msomaji wa Qur'an: Qur'an Tukufu kwa ajili ya Ufunguzi wa Majlisi, imetolewa na Mwanafunzi wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa)aitwaye: Zulekha ambaye amesoma Aya Tukufu zinazohusiana na subira, haki, na makemeo dhidi ya dhuluma. Kwa hakika ni Aya zinazoongeza kina cha kiroho katika hafla hiyo ya Maombolezo.

Madrasat Hazrat Zainab(as) Kigamboni: Katika mwendelezo wa Maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein(a.s)  | "Baada ya Shahada ya Imam Hussein(as)" +Picha

"Matam" na Mashairi ya Huzuni: Majlisi iliambatana na zoezi la Matam na Mashairi ya Huzuni ya Maombolezo. Na hili ni suala linalohusisha taratibu za maombolezo ya kitamaduni, kama vile kupiga vifua (Ma'tam) au kuonyesha hali ya majonzi kwa njia nyingine, na imefanywa kwa ushirikiano wa wanafunzi wote. Hii ni sehemu muhimu ya kuonyesha hisia za huzuni na kuheshimu msiba huu mkubwa wa Karbala.

Madrasat Hazrat Zainab(as) Kigamboni: Katika mwendelezo wa Maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein(a.s)  | "Baada ya Shahada ya Imam Hussein(as)" +Picha

Muda wa Mjalisi: Majlisi hii imedumu kwa muda wa saa moja (dakika 60) ambazo zimetosha kabisa kuanza Programu nzima mwanzo hadi mwisho. Na huo ndio muda wa Majlisi zote katika masiku haya ya Maombolezo ya Muharram, ambao unatosha kabisa kwa ajili ya kutoa taarifa na maombolezo kwa ufanisi ndani ya muda uliopangwa.

Wasimamizi wa Programu hii: Wanafunzi Mabinti wa Hawza ya Hazrat Zainab (sa)

Your Comment

You are replying to: .
captcha