"Kisasi chetu hakilali, na siku za giza zinakungojeeni. Hutaonja usalama baada ya leo," Mahdi al-Mashat, Rais wa Yemen alitoa indhari hiyo katika hotuba yake ya jana Jumamosi.
Ameeleza bayana kuwa, "Damu ya Mashahidi hawa wakuu itakuwa chachu na motisha zaidi kwa ajili ya kusimama kidete, kuwa na uthabiti, ustahimilivu, na kujitolea," akiahidi kwamba taifa hilo litaendelea kuimarisha vikosi vya jeshi lake.
"Hutaweza kuvunja uthabiti wetu kwa sababu tuko pamoja na Allah. Heshima yetu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kufa shahidi, na ahadi Yake ya uhakika kwetu ni ushindi usioepukika," afisa huyo amesisitiza. Rais wa Yemen ameongeza kuwa, mashahidi hao wa Yemen wamelipa gharama ya kusimama dhidi ya “maadui wakubwa zaidi wa Mwenyezi Mungu, yaani Wazayuni watenda jinai.”
Matamshi hayo yametolewa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel katika mji mkuu wa Yemen kupelekea kuuawa shahidi Waziri Mkuu wa wa Serikali ya Kitaifa ya Mabadiliko na Ujenzi ya nchi hiyo, Ahmed Ghaleb Al-Rahawi na maafisa wengine walokuwa wakihudumu katika nyadhifa mbalimbali.
Mashambulizi hayo yametokea huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukishadidiisha hujuma zake za kinyama dhidi ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu.
Mashambulizi hayo yalianza baada ya wanajeshi wa Yemen kuanza kufanya operesheni za karibu kila siku dhidi ya shabaha nyeti za Israel, ili kukabiliana na vita vya mauaji ya halaiki ambavyo Tel Aviv ilianzisha dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 2023.
Your Comment