Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa Iran inahitajika katika juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (Daesh) nchini Iraq na Syria.
Bwana Kerry ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba muungano kwa minajili ya kupambana na kundi la kigaidi la Daesh una majukumu mengine mengi mbali na hatua za kijeshi na kwamba yamkini Jamhuri ya kiislamu ya Iran itaombwa itoe msaada wake katika kupambana na magaidi.
20 Septemba 2014 - 09:07
News ID: 638836

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa Iran inahitajika katika juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (Daesh) nchini Iraq na Syria.