19 Novemba 2014 - 16:26
Serikali ya Israel  yalipa kisasi kwa kubomoa nyumba ya mpalestina aliyeshambulia kituo cha treni

Serikali ya Israel imebomoa nyumba ya mpalestina aliyefanya mashambulizi katika kituo cha treni na kuua watu watatu.

Serikali ya Israel imebomoa nyumba ya mpalestina aliyefanya mashambulizi katika kituo cha treni na kuua watu watatu.

  Waumini wa kiyahudi wamenza kurejea kwa ibada katika sinagogi lililoshambuliwa jana mjini Jerusalem huku wapalestina wakijiandaa kushuhudia hatua kali kutoka Israel kama kisasi cha Israel kwa wapalestina,huku mzozo kati yao ukizidi kufukuta

  Waumini wa kiyahudi wamerejea kusali katika sinagogi hilo lililoshambuliwa hapo jana na wapalestina wawili ambao waliwaua watu wanne na askari mmoja kwa kutumia bunduki na mashoka.Mmoja wa waumini hao Gavriel Cohen amesema shambulizi hilo la jana linaonyesha kuwa hatma yao ya baadaye inategemea mipango ya mwenyezi Mungu.

  Waziri mkuu wa Israel ameapa kuchukua hatua kali kukabiliana na ongezeko la visasi vya mashambulizi kutoka kwa wapalestina yanayowalenga waisrael.Na siku moja baada ya tamko hilo, maafisa wa usalama wa Israel wamebomoa nyumba ya mpalestina aliyewaua watu watatu mwezi uliopita katika shambulizi lililowalenga abiria waliokuwa wakisubiri kuabiri treni kituoni mjini Jerusalem.

Jeshi na polisi la Israel limetoa taarifa inayosema wameyabomoa makaazi ya Abdel Rahman Shaloudi leo alfajiri. Shaoludi kijana wa umri wa miaka 21 aliuawa na askari alipokuwa akijaribu kutoroka baada ya kuwagonga kwa gari lake abiria kituoni.

Ghasia zimeongezeka mjini Jerusalem na maeneo mengine nchini Israel tangu mwezi Julai kufuatia kuchomwa moto  msikiti na vitabu vya kiislamu hadi kuuawa kwa kijana wa kipalestina na washambuliaji wa kiyahudi na baadaye mashambulizi ya kulipiza kisasi yakasababisha vifo vya vijana watatu wa kiisrael yaliyosababisha Israel kuushambulia kwa ukanda wa Gaza kwa siku hamsini.

   Jeshi la Israel lilikuwa likibomoa au kuripua makaazi ya wanamgambo kwa miongo kadhaa lakini liliacha mwaka 2005 kwa kugundua haikuzuia mashambulizi dhidi ya Israel lakini limerejea kuzibomoa nyumba za washambuliaji kama njia ya kuwaadhibu washambuliaji na jamaa zao.

Kitendo hiki cha Israel kubomoa nyumba za watu na kuadhibu familia nzima kwa kuwasababishia kutokuwana makazi, kinafasiliwa kama hatua ya kijinga inayofanywa na utawala wa Israel.

  Netanyahu ameahidi kuharakisha ubomoaji wa makaazi ya washambuliaji waliofanya mashambulizi yote ya hivi karibuni mjini Jerusalem kuambatana na sera iliyoanzishwa tena mapema mwezi huu.

Ubomoja ni ukiukaji wa haki za kimataifa, Israel imekuwa ikiuwa waparestina wengi wasio na hatia kwa kulipa kisasi cha kuuawa muisrael mmoja,  hatua hii pia inaonekana ni kinyume na haki za binadamu.

   Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelaani sera hiyo ya Israel kama adhabu inayowalenga sio tu washambuliaji bali familia zao ambao hawana hatia. Shirika la Amnesty International limesema kuziboma nyumba za familia za washambuliaji ni ukiukaji wa haki za kimataifa.

Shambulizi la jana katika sinagogi ndilo baya zaidi kuwahi kushuhudiwa mjini Jerusalem tangu mwaka 2008 ambapo mpalestina aliyekuwa na bunduki aliwaua watu wanane katika shule ya kidini.

Palestina inaitaka Israel kuikabidhi maeneo ya Jerusalem,ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi maeneo yaliyonyakuliwa kwa nguvu na Israel baada ya vita vya mwaka 1967 ambayo kihistoria ni haki ya waparestina.

Huku hayo yakijiri, bunge la Uhispania hapo jana jioni lilipiga kura kwa wingi kutaka Palestina kutambuliwa kama taifa huru.Wabunge 319 dhidi ya wawili walipiga kura kuitambua Palestina na kuitaka serikali ya waziri mkuu Mariano Rajoy kuitambua rasmi Palestina kwa kusema hiyo ndiyo suluhisho pekee ya kuumaliza mzozo wa mashariki ya kati.

Yafaa kuashiria kwamba Israel imekuwa ikikiuka haki za binadamu na kuvunja mikataba ya amani kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua.

Tags