29 Novemba 2014 - 19:31
Mahakama yamfutia mashtaka ya mauji dikteta Hosn Mubarak

Mahamakama ya Misri imemfutia dikteta Hosn Mobarak mashtaka ya mauaji ya waandamanaji wa mwaka 2011.

Mahamakama ya Misri imemfutia dikteta Hosn Mobarak mashtaka ya mauaji ya waandamanaji wa mwaka 2011.

 Aliyekuwa Rais wa Misri Dikteta Hosni Mubarak amesema hakufanya  makosa yoyote baada ya mahakama hii leo kumfutia mashitaka ya mauaji ya waandamanaji waliopelekea kung'olewa kwake madarakani wakati wa wimbi la uasi mwaka 2011. Akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha televisheni,kutoka hospitali ya kijeshi ambako anahudumia kifungo cha miaka mitatu cha hukumu ya kesi nyingine ya ufisadi,Mubarak amesema kamwe hakufanya makosa yoyote. Uamuzi huo wa mahakama pia umewaondolea mashitaka makamanda waandamizi sita wa usalama waliohudumu wakati wa uongozi wa Mubarak. Jaji Mahmud Kamel al Rashidi amesema ni historia na Mungu tu ambaye anaweza kutoa hukumu kwa mtu aliyehudumu kama kiongozi wa Misri kwa zaidi ya miaka 30. Dikteta Hosn mobarak anakabiliwa na mashataka mengine ya ufisadi wa mali ya umma ambapo alikuwa akuuza rasilimali ya gesi ya nchi hiyo kwa utawala wa Israel kwa bei ya chini kuliko bei ya gesi ya soko la dunia.

  Wannchi wa Misri wameonyesha kutoridhishwa na hukumu ya mahakama hiyo, na kuomba uadilifu utendeke kwani waandamaji hao waliuawa kwa amri ya dikteta huyo.

 

 

Tags