3 Desemba 2014 - 19:46
Sheikh wa Chuo cha Azhar aomba watu wapambane dhidi ya wanaochafua jina la uilsamu

Sheikh Mkuu wa Al-Azhar nchini Misri, Ahmed al-Tayeb, ameutolea wito muungano wa kimataifa unaopambana na kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria, kutanua vita vyake na kuyajumuisha makundi mengine yote yanayochafua jina la Uislamu.

 Akizungumza kwenye kongamano la kukabiliana na ugaidi mjini Cairo hivi leo, Sheikh Tayeb amesema muungano huo wa kimataifa unapaswa kuelekeza nguvu zake hadi kwa taasisi na mataifa yanayounga mkono makundi ya kigaidi. Chuo Kikuu cha al-Azhar ni moja ya taasisi kongwe kabisa na zinazoheshimika sana miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni duniani. Kundi la kigaidi la Daesh lilijitangazia utawala wake kwenye eneo la Syria na Iraq, kufufua ukhalifa uliokuwapo zaidi ya miaka 1,000 iliyopita. Lakini vitendo vyake vya kuuwa, kutesa na kuwatia utumwani watu wasio hatia, vimelifanya likataliwe na sehemu kubwa ya Waislamu duniani.

Yafaa kuashiria kuwa kongamano lingine la kupinga wanaochafua jina la dini tukufu ya kiislamu lilifanyika katika Jamhuri ya kiislamu ya Iran tarehe  24 Novemba 2014 katika mji mtukufu wa Qum ambao ni makao makuu ya elimu ya madhehebu ya kiislamu ya Shia ithna asharia.

Tags