5 Desemba 2014 - 18:44
Raia wa Ujeruman ahukumiwa kifungo kwa kosa la kujiunga na magaidi wa Daesh + Picha

Raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 20 leo amehukumiwa kifungo cha miaka 3 na miezi tisa jela baada ya kukiri kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh Syria. Kesi hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanyika Ujerumani kuhusu Mjerumani

Raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 20 leo amehukumiwa kifungo cha miaka 3 na miezi tisa jela baada ya kukiri kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh Syria.

Kesi hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanyika Ujerumani kuhusu Mjerumani anayetuhumiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi. Majaji wametoa uamuzi wa kumshughukia kijana huyo anayefahamika kama Kreshnik B mzaliwa wa Ujerumani mwenye asili ya Kosovo kama mtoto kutokana na kwamba hajakomaa.Kijana huyo alikaa kwa muda wa miezi sita nchini Syria mwaka jana lakini mahakama imesema hakuna ushaidi kwamba alishiriki moja kwa moja vitani.

Yafaa kuashiria kwamba wapambanaji wengi kutoka nchi za ulaya wamekwenda Syria kumbana wakishirikiana bega kwa bega na magaidi wa Daeshi ili kuangusha serikali ya Syria na Iraq, watu hawa wameanza kurejea makwao baada ya kuhelemewa katika vita na kuona kuwa uwezekano wao wa kushinda ni mchache hasa baada ya majeshi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kuingia vitani kuzisaidia  serikali za Syria na Iraq, wapambanaji hawa wanaorejea nchini kwao wanakamatwa kwani wanaonekana kuwa ni tishio kubwa kwa usalama na amani za nchi zao.

 

Tags