Wajerumani wameandamana kuonyesha wasiwasi wao dhini ya waislamu wanaoishi katika nchi yao,kwa kuhofia matukio ya kigaidi.
Si raia wa ujerumani tu bali watu wengi wa ulaya wanatawaliwa na hofu juu ya uislamu.
Hii inatokana na baadhi ya makundi ya kiislamu kufanya jinai na kuzinasibisha na dini tukufu ya kiislamu na kwamba wanafanya hayo kwa ajili ya uslamu.
Kwa mfano: kutokea mashambulizi ya Septemba 11 na khofu ya daima dhidi ya Uislamu, mijadala juu ya kofia na baibui za nikabu, mauaji yanayofanywa na kundi la kusuni la Daesh huko Iraq na Syria, ambapo Waislamu wa Kijerumani wenye asili za kigeni wamekwenda kujiunga nalo kama wapiganaji wa jihadi, wimbi la wakimbizi kutoka nchi ambazo zinakabiliwa na mashambulizi ya Daesh, na suala lililochukuwa muda mrefu la ikiwa nchi yenye Waislamu wengi Uturuki, iruhusike kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya ama la.
Watu wengi wameelemewa na hayo na hilo linaweza kufahamika, kwa sababu ukiacha uchambuzi wa kisomi kwenye siasa na vyombo vya habari, watu wengi hawana uwezo wa kuchambua tafauti kati ya taswira hiyo inayombatanishwa na Uislamu na Uislamu halisi. Kwao wao kila Muislamu ni kama Muislamu mwengine.
Wakati huo huo, vyombo vya habari vinazidi kuzifanya hisia hizo kuwa kali. Mfano halisi ni tukio la hapo jana la mkahawa kutekwa nyara mjini Australia. Hata kabla ya taarifa za ndani kujuilikana, tayari habari nzima ilishapagazwa majina yale yale: "jihadi", "mpiganaji wa Mungu", "Muislamu mwenye siasa kali." Hakuna maneno ya kutafautisha ukweli mmoja kutoka mwengine. Na katika hali ya kawaida, hilo linachanganywa na kauli ya hivi karibuni ya Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki, ambaye aliwashauri Waturuki wanaoishi hapa Ujerumani kutojiona Wajerumani sana.
Hisia dhidi ya uislamu ziliendelea baada ripoti juu ya vijana kutoka Wuppertal waliokuwa wakijiita "polisi wa Sharia" ambao wakitembea mjini na kuwataka wanawake wavae mavazi sahihi ya Kiislamu
Tatizo la Ujerumani ni kwamba kuna watu wengi wanaoyahofia hayo lakini hakuna mjadala wa wazi kwayo. Na watu wengi, kwa hivyo, wanajihisi kwamba hisia zao hazipewi uzito. Badala yake wanabezwa hata kwenye kiwango cha watunga sera. Mfano wa karibuni ni kauli ya Waziri wa Sheria wa Ujerumani, Heiko Maas, ambaye ameyaita maandamano ya Dresden kuwa ni "aibu kwa Ujerumani".
Kauli hii ni ishara mbaya kabisa ya kuwatenga watu na inaonesha kwa kiasi gani namna uwelewa wa jambo hili ulivyopewa umuhimu mdogo, kwani hata kwenye chama chake Maas mwenyewe, kuna sauti nyingi zinazounga mkono mawazo ya Pegida.
Asilimia 46 ya walioulizwa kwenye chama hicho cha SPD walisema wanaakisi matakwa ya Pegida. Wanasema kuwa SPD si chama ambacho hisia za waumini wa Ukristo zinazingatiwa. Na hilo ni jambo la kufanyiwa kazi, maana matokeo yake ni kwamba makundi yenye siasa kali za mrengo wa kulia yanaweza kuwavutia wengi miongoni mwa raia.
Pamoja na kuwepo makundi ya kislamu ya dhehebu la Sunni yanayofanya jinai na kuzinasibisha na uislamu, hii haimaanishi kuwa dini ya kiislamu ni mbaya, kwani tunashuhudia katika nchi ya Afrika ya kati kumetokea makundi ya Ant Baraka ambayo yanaua waumini wa kiislamu, pia kumetokea jinai kadhaa za maaskofu kubaka na kuwanajisi watoto, kuna jinai zinazofanya na taifa la dini ya kiyahudi la Israel dhini ya haki za binadamu na mengine mengi, hizi zote hazitoshi kuwa dalili ya kuichafua dini kwani matendo ya watu ni yanayoenda tofauti na mafunzo ya dini hayafai kunasibishwa na uhalisia wa dini.
Vyombo vya habari vingi pia vimechangia katika kuchafua jina la dini ya uislamu kwani ikitokea tukio la lolote hawaangalii watu waliotenda tukio kama majambazi au watu waovu bali wanawataja kwa kutazama dini zao.
Kwa mfano tukio la kuvamiwa mgahawa wa Sydney ambapo wavamizi walikuwa watatu mmoja wao ni muislamu, vyombo vya habari vimemuongelea huyu muislamu zaidi.
Katika kipindi ambacho jinai zikifanywa na wakristo au mayahudi hawatambulishwi kwa dini zao.
Watu inabidi wajue kutofautisha kati ya tende na mkaa, wajue tofauti kati ya anayejiita muislamu na uislamu halisi,tofauti kati ya askofu na ukristo, tofauti kati ya jinai za Israel na dini ya uyahudi.