Kiongozi mmoja wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab amejisalimisha nchini Somalia. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa idara ya ujasusi ya Somalia, kiongozi huyo ambaye ni Zakariya Hersi alijikabidhisha kwa polisi katika mkoa wa Gedo, mashariki mwa nchi. Hersi ni mmoja kati ya viongozi wanane wa juu kabisa wa Al-Shabaab waliokuwa wakisakwa kwa nguvu. Inaaminika kwamba alikuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi na fedha. Serikali ya Marekani ilikuwa imeahidi kutoa zawadi ya dola milioni tatu kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake. Kundi la Al-Shabaab limeweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani lakini bado linatishia amani katika maeneo mbalimbali nchini Somalia na Kenya.
27 Desemba 2014 - 18:19
News ID: 661081

Kiongozi mmoja wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab amejisalimisha nchini Somalia.