19 Januari 2015 - 11:58
Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu amani ya Ukraine

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu mapigano makali yanayoripotiwa mashariki mwa Ukraine katika uwanja wa ndege wa Donetsk na kutaka ghasia hizo kukomeshwa mara moja

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu mapigano makali yanayoripotiwa mashariki mwa Ukraine katika uwanja wa ndege wa Donetsk na kutaka ghasia hizo kukomeshwa mara moja. Hapo jana kuliripotiwa mapigano makali kati ya wanajeshi wa serikali ya Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi wanaotaka kujitenga kwa eneo hilo la mashariki mwa Ukraine katika uwanja huo muhimu wa ndege huku jeshi likitangaza limeweza kuchukua sehemu kubwa ya uwanja huo kutoka mikononi mwa waasi. Katika taarifa aliyoitoa hapo jana Ban amesema anatiwa wasiwasi na kuongezeka kwa mapigano hayo na kuongeza yanatishia kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi Septemba mwaka jana. Kiasi ya watu 14 wakiwemo wanajeshi wanne waliuawa katika mapigano hayo ya mwishoni mwa juma, makaazi kadhaa yaliharibiwa na umeme kukatizwa.

Tags