Mapigano mashariki mwa Ukraine yameendelea, huku serikali mjini Kiev ikidai kwamba Urusi imetuma mamia ya wanajeshi kwenye eneo la mpakani, ili kuwasaidia waasi wanaowania kujitenga. Wakaazi wamesema mashambulizi makubwa ya makombora katika mji wa Donetsk yaliliharibu kabisa soko na hospitali ya mji huo ambapo watu walibidi kuhamishwa. Wakati huo huo Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kutokuweko na mabadiliko yoyote, katika sera ya umoja huo kuelekea Urusi. Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini ameonya kwamba hali imekuwa mbaya zaidi. Mogherini amesema wataendelea na msimamo wao hadi Urusi itekeleze makubaliano ya amani yaliofikiwa mwezi Septemba. Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alisema jana kwamba juhudi za kuandaa mkutano wa kilele zikihusika Urusi, Ukraine na Ujerumani zitaendelea.
20 Januari 2015 - 11:24
News ID: 665927

Mogherini amesema wataendelea na msimamo wao hadi Urusi itekeleze makubaliano ya amani yaliofikiwa mwezi Septemba.