Marekani na Cuba zinaanza mazungumzo ya kihistoria leo kuhusu kurejesha mahusiano ya kidiplomasia baada ya kikao kilichojadili masuala ya uhamiaji kudhihirisha changamoto zilizopo katika kuondokana na uhasama wa nusu karne kati ya nchi hizo. Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kwenda Cuba katika kipindi cha miaka 35 utakamilisha mazungumzo ya siku mbili leo mjini Havana, huku pande zote mbili zikionya hakuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya haraka. Maafisa wa Marekani wanasema wana matumaini Cuba itakubali kuzifungua balozi zake na kuwateua mabalozi katika miji mikuu Washongton na Havana katika miezi ijayo. Marekani inataka pia vikwazo vya kusafiri vilivyowekewa wanadiplomasia wake viondodolewe na iruhusiwe kusafirisha vifaa na mahitaji kwa tume ya mjini Havana.
22 Januari 2015 - 12:57
News ID: 666429

Marekani na Cuba zinaanza mazungumzo ya kihistoria leo kuhusu kurejesha mahusiano ya kidiplomasia baada ya kikao kilichojadili masuala ya uhamiaji kudhihirisha changamoto zilizopo katika kuondokana na uhasama wa nusu karne kati ya nchi hizo.