Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya ndani ya Misri imetangaza kufanikiwa kuzuia kutokea kwa mripuko uliokuwa umepangwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo, baada ya msako mkubwa uliofanywa dhidi ya magaidi na kufanikiwa kusambaratisha mashambulio ya kigaidi yaliopangwa na kikundi hicho dhidi ya wakristo wa Asyut nchi humo.
Aidha wizara hiyo imetangaza kuwa, majeshi ya Misri yamefanikiwa kuwaangamiza magaidi 7 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambao ni katika magaidi walikuwa wamepanga kufanya shambulio la kigaidi katika sehemu ya Saumah na kuwashambulia wakristo wanaoishi sehemu ya Asyut nchini humo.
Magaidi hao 7 walikuwa wakifuatiliwa na vyombo vya uasalama nchini humo, ambapo baada ya vyombo hivyo kuvamia katika sehemu zao za maficho ziliopo katika sehemu za milima iliokuwa katika mkoa wa Asyut na hatimaye kuwaangamiza.
Nchi ya Misri hivi mwishoni imepatwa na miripuko miwili ya kigaidi katika wilaya ya Tantai, ambapo imepelekea kuuwawa kwa watu 45 na wengine 125 kujiruhiwa katika makanisa ya sehemu hiyo.
Baada ya kutokea kwa mashambulio hayo, kikundi cha kigaidi cha Daesh kilitangaza kupanga mashambulizi hayo.
Katika kauli ya wizara ya mambo ya ndani nchini humo imetangazwa kuwa; vyombo vya usalama vya nchi hiyo walishambulia maficho yao katika milima ya Arabul-Awamir katika mkoa wa Asyut na baada ya mapigano makali na magaodi hao, ndipo wakafanikiwa waangamiza magaidi hao saba.
Aidha majeshi ya Misri yamefanikiwa kuteka silaha na vifaa vingine vya vita kutoka mikononi mwa kikundi hicho nchini humo.






mwisho/290