Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waandamanaji wanaounga mkono jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania wameshambuliwa vikali na Polisi walipokuwa wakiandamana kupinga viongozi wao 12 kufikishwa mahakamani. Polisi hao wa kuzuia fujo walitumia virungu kuwakabili watu hao walioandamana katika mji wa Barcelona. Waandamanaji hao walizuia usafiri wa reli katika stesheni ya Plaza Catalunya. Maandamano hayo yalianza kama mgomo uliondaliwa na wanafunzi pamoja na vyama vya wafanyakazi vinavyounga mkono kujitenga kwa Catalonia. Jimbo la Catalonia lilijitangazia uhuru wake mwaka 2017 baada ya kuitishwa kura ya maoni ambayo haikutambuliwa na mahakama kuu ya Uhispania. Viongozi hao 12 walikamatwa baadae mwaka huo. Tisa kati yao wamewekwa ndani bila ya dhamana wakisubiri kufunguliwa mashtaka. Ikiwa watapatikana na hatia ya uasi, uchochezi na matumizi mabaya ya fedha za umma wanaweza kupewa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 25 jela kila mmoja.
Nchi za Ulaya zimekaa kimya juu ya hali hii na badala yake kuingilia mambo ya ndani ya Venezuela na kumtambua mpinzani kuwa ndio rais halali.
Mwisho wa habari / 291