(ABNA24.com) Ripoti mpya ya Unicef imesema, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) inaongoza kwa ndoa za utotoni duniani hususan kwa upande wa wavulana.
Ripoti hiyo imeiorodhesha CAR kuwa inaongoza kwa ndoa hizo kwa asilimia 28, ikifuatiwa na Nicaragua asilimia 19 na Madagascar ikishika nafasi ya tatu kwa asilimia 13.
Akizungumzia ripoti hiyo iliyotolewa leo Ijumaa, Henrietta Fore, Mkurugenzi Mkuu wa Unicef amesema "ndoa za mapema zinawapokonya watoto maisha ya utotoni'.
Ripoti hiyo ya Unicef imesema, katika watoto bilioni 2.2 duniani, milioni 765 miongoni mwao hivi sasa wako katika ndoa za utotoni. Ripoti ya Unicef inasema kuwa, binti mmoja kati ya watano kote duniani analazimishwa kuingia kwenye ndoa kabla ya kutimiza miaka 18, ikilinganishwa na mvulana mmoja kati ya 30.
Unicef imewataka viongozi wa dunia kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi waliyotoa ya kutokomeza ndoa hizo duniani kufikia mwaka 2030, chini ya Malengo ya Maendeleo-Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDG's .
.........
300