-
Ibada za kufanya Usiku wa 23 wa Lailatul-Qadri
Inapendekezwa kusoma Dua ya (......يا مُدَبِّرَ الاُمُورِ ) hali ya kuwa umerukuu, umesujudu, umesimama, umekaa na irudierudie kila sehemu, na isome hata kila siku na iombe Dua hii kwa wingi katika Usiku wa mwisho wa Ramadhani Tukufu.
-
Mgogoro wa Kibinadamu huko Gaza; Papa Francis ametoa wito wa kusitishwa kwa kudumu kwa mapigano huko Gaza
Akielezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu huko Gaza, Papa Francis amesisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kukabiliana na mgogoro huu na kusaidia watu wasio na hatia.
-
"Atasamehewa Dhambi Zake Zilizotangulia"
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Imepokewa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwamba amesema:" "مَنْ قَامَ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ" "Atakayesimama (kuswali na) kuhuisha Usiku wa Laitatul - Qadr kwa imani na kutarajia malipo, atasamehewa dhambi zake za zilizotangulia". المصدر: فضائل الأشهر الثلاثة: 136 / 144 Rejea: Fadhail al_Ash-huri al_Thalatha: 136 / 144.
-
Mashambulizi ya anga ya Marekani nchini Yemen yameingia wiki ya pili / Mashambulio makubwa ya mabomu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hodeidah
Mji wa Hodeidah ulioko Magharibi mwa Yemen umelengwa na mashambulizi makubwa ya mabomu ya jeshi la Marekani.
-
Wosia Kwa Historia na Wanadamu Wote
Wosia wa Hadhrat Ali (amani iwe juu yake), ni moja ya maandiko muhimu ya Kiislamu yaliyosheheni mafunzo ya kimaadili (kiakhlaq), kijamii na kisiasa, na sio tu kwa ajili ya watoto na masahaba zake, bali pia ni nuru kwa watu wote wanaotafuta ukweli (uhakika) na uadilifu.
-
Mashahidi 38 wa Kipalestina; Uovu mpya wa utawala wa Kizayuni huko Gaza
Katika muendelezo wa mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni umeua idadi nyingine ya Wapalestina.
-
Infographic | Aamali za Usiku wa 23 wa Mwezi wa Ramadhani
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) - Abna-: Usiku wa Lailatul-Qadr ni Usiku ambao hakuna Usiku mwingine katika mwaka mzima unaofikia ubora wake, na kitendo cha usiku wa Lailatul-Qadr kinakuwa ni bora zaidi kuliko kitendo cha Miezi elfu moja. Katika Usiku wa Lailatul-Qadr, mipango (makadirio) ya kila mtu kwa mwaka mzima inatathminiwa (nakupangwa au kukadiriwa). Katika Usiku wa Lailatul-Qadr, Malaika na Ruhu, ambaye ni Malaika mkubwa zaidi, kwa idhini ya Mola, humtumikia (huwa katika khidma kwa) Imam wa Zama (a.t.f.s), ambapo hushuka na kuwasilisha hatima (makadirio au) ya kila mtu kwa Imam (a.t.f.s).
-
Asilimia 30 ya ongezeko la idadi ya Mazuwwari kwenye Madhabahu (Haram) ya Imam Ali (AS) katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Idadi ya Mazuwwari wa Madhabahu ya Imam Ali (AS) iliweka rekodi katika siku ya 21 ya Ramadhani, na mwaka huu, mahujaji milioni moja na 500,000 zaidi wametembelea (wamezuru) Madhabahu ya Alawi kuliko mwaka jana.
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi nchini Iraq katika mazungumzo na Abna:
Kuhifadhi Utukufu wa Ramadhani na kuimarisha matumaini, ni sababu ya Nguvu na Ukaribu wa Kiislamu
Ayatollah Hosseini, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Iraq na mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi ameashiria taathira za funga kiutamaduni na kijamii na kusisitiza juu ya ulazima wa kuhifadhi utukufu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika jamii.
-
Sababu ya Ushujaa na Ujasiri wa Ali bin Abi Talib (a.s)
Sheikh Said Othman: "Imam Ali (a.s) anakumbukwa na Ulimwengu wote wa Kiislamu kuwa yeye ni Shujaa wa Kiislamu, aliyeupigania Uislamu, na kuuhami Uislamu kwa ushujaa wake na ujasiri wake, daima aliutetea uhai wa Uislamu na aliuheshimisha Uislamu kupitia Upanga wake, kama ambavyo Ummul - Muuminina Khadija (s.a) aliuhamia na kuuheshimisha Uislamu kupitia Mali yake".
-
Mayahudi shari ndio chaguo lao, na kuangamizwa ndio hatima yao
Sheikh Mselem: "Mayahudi walikuwepo Madina. Lakini walileta ukorofi na kibri, wakawa wakivunja makubaliano waliyokuwa wakiingia na Mtume (s.a.w.w). Mtume (s.a.w.w) akawatandika na kuwatimua kutoka katika Bara Arabu">
-
Ayatollah Ramezani: Kutokushindwa ndio msingi wa utawala wa Alawi; Imam Ali (amani iwe juu yake) ni kielelezo cha Ulimwengu wa Mwanadamu
Katibu Mkuu wa Baraza la Kidunia la Ahlul-Bayt (a.s.) katika hafla ya kuhuisha Usiku wa 21 wa Ramadhani, akiashiria kwamba kutokukubali ndio msingi wa utawala wa Alawi, alisema: Imam Ali (a.s) ni kielelezo cha ulimwengu wa Wanadamu.
-
Ripoti ya Picha | Maandamano ya Maombolezo ya kuuawa Shahidi Amirul Muuminina (AS) yaliyohudhuriwa na Ayatollah Vahid Khorasani
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Sambamba na kumbukumbu ya Kifo cha Kishahidi cha Amirul Muuminina (AS), Maandamano ya maombolezo yamefanyika yakihudhuriwa na Ayatollah Al-Udhma Hossein Vahid Khorasani ambaye ni katika Marajii Taqlid wa Ulimwengu wa Shia Ithna Ashari. Maandamano haya ya maombolezo yameanzia nyumbani kwa Marjii huu Taqlid hadi kwenye Haram Tukufu ya Hazrat Fatima Maasoumah (s.a).