-
Dunia ikiwa kwa ajili yako, na ikiwa dhidi yako
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -Abna-; Imam Ali bin Abi Talib (a.s) anasema kuhusu uhakika wa Dunia: "Dunia inapomgeukia mtu (na ikawa upande wake na kwa ajili yake), basi humkopeshe mema na mazuri ya wengine, lakini dunia hii hii inapomgeuka mtu (huyo na kuwa dhidi yake), huchukua (hundoka toka kwa mtu huyo; tena kwa kumpokonya na kuyachukua) mazuri yote na mema yake mwenyewe".
-
Mawakili 77 wa Ujerumani waitaka serikali iheshimu hukumu ya ICC ya kumkamata Netanyahu
Mawakili 77 mashuhuri wa Ujerumani wametoa tamko la kuunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kuagiza waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe na kuitaka serikali ya shirikisho ya Ujerumani iheshimu uamuzi huo.
-
Peskov: Ulaya inashadidisha mzozo wa Ukraine kwa kuzidisha misaada yake ya kijeshi kwa nchi hiyo
Msemaji wa ikulu ya Russia (Kremlin) ametangaza kuwa Ulaya inachagiza mzozo wa UKraine kwa kuzidisha misaada ya kijeshi kwa nchi hiyo badala ya kutatua vyanzo vya mzozo huo.
-
Mapatano mapya ya nchi za Umoja wa Ulaya dhidi ya Russia
Kwa kutilia maanani jaribio la utawala wa Trump la kuanzisha usitishaji vita nchini Ukraine kwa kuilazimisha ikubali masharti yaliyowekwa na Russia na upinzani wa nchi za Umoja wa Ulaya dhidi ya suala hili, na kwa upande mwingine madai ya baadhi ya viongozi wa Ulaya kuhusu vitisho vya Russia dhidi ya bara hilo, nchi hizo sasa zimechukua hatua mpya kwa ajili ya kukabiliana na Moscow.
-
Mchambuzi: Kurukia vita baada ya vita ni 'muhimu' kwa Netanyahu kubaki madarakani
Elijah Magnier, mchambuzi mashuhuri wa masuala ya kijeshi amesema, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu anafanya juu chini ili aweze kusalia madarakani kwa angalau miaka miwili mingine; na hiyo ndiyo sababu ya "kurukia vita baada ya vita".
-
Hamas; kuuawa shahidi Barhoum; jinai nyingine katika rekodi nyeusi ya utawala wa Kizayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa na kutoa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Esmail Barhoum mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo.
-
Siku ya saba ya uvamizi wa Israel wa Ghaza; makumi wauawa na kujeruhiwa
Utawala wa wa Kizayuni wa Israel Israel unaendelea kufanya jinai na mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza ambapo tangu asubuhi ya leo hadi wakati tunaandaa taarifa hii, makumi ya Wapalestina wamekuwa wameshauwa shahidi na kujeruhiwa, leo ikiwa ni siku ya saba ya tangu kuanza wimbi jipya la jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
-
Chombo cha Kizayuni: Kuna ukosefu wa kutoaminiana kitaasisi Israel
Chombo kimoja cha habari cha lugha ya Kiebrania kimechapisha makala inayofichua mzozo mkubwa wa kutoaminiana ndani ya muundo wa mamlaka na kiutawala huko Israel.
-
Kamanda: Jeshi la Iran litawaponda maadui wakifanya kosa lolote
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Kiumars Heidari amesema kikosi chake kiko macho na tayari kabisa kuwaangamiza maadui endapo watathubutu kufanya makosa yoyote dhidi ya taifa hili.
-
Diplomasia hai ya Iran katika kukabiliana na migogoro inayoibuliwa na utawala wa Kizayuni katika eneo
Seyyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia matukio ya eneo, yakiwemo ya Palestina na Yemen katika mazungumzo yake ya simu na Mawaziri wenzake wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia na Misri na kubadilishana nao mawazo jinsi ya kukabiliana na migogoro inayoibuliwa mara kwa mara na utawala wa Kizayuni katika eneo.
-
Iran yatahadharisha kuhusu athari za vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon kwa usalama wa dunia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuhusu taathira za vita vipya vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon kwa usalama na amani ya kimataifa.
-
Iran: Tuko imara! Hakuna mtu anayeweza hata kufikiria kuanzisha vita dhidi yetu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Majeshi na serikali yetu tumeijengea nchi kinga ya kutosha kiasi kwamba hakuna hata mtu anayeweza kufikiria kuanzisha vita dhidi ya Iran."
-
Pezeshkian: Marekani haiwezi kulikwamisha taifa la Iran katika jambo lolote
Rais Masoud Pezeshkian amesema kwamba Marekani haiwezi kuiwamisha Iran katika jambo lake lolote lile iwapo taifa hili la Kiislamu litashikamana vilivyo na mafundisho ya Qur'ani na ya Uislamu.
-
Ripoti ya Picha | Hafla ya Kuhuisha Usiku wa Mwisho wa Lailatul- Qadr Katika Haram Tukufu ya Hadhrat Maasoumeh (s.a) - Qom
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (A.S.) - Abna - Hafla ya kuhuisha Usiku wa 23 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilifanyika katika Madhabahu Tukufu ya Hadhrat Fatima Maasoumeh (SA) katika Mji Mtukufu wa Qom kwa kuhudhuriwa na wapenzi na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) isma na utoharifu (amani iwe juu yao).
-
Jopo la Wanawake la Kongamano la 6 la Kimataifa la Quds Tukufu litafanyika
Kongamano hili lenye jina la "Tuelekee Al-Quds" litafanyika siku ya Jumanne, tarehe 25 Machi, 20205 Jijini Tehran, katika jengo la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS).
-
Video | Usiku wa Upweke na wa Kustaajabisha wa Lailatul-Qadr Katika Haram Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a)
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; Wakati katika miaka ya nyuma Hafla za kuhuisha Usiku wa Lailatul Qadr zilikuwa zikifanyika katika Madhabahu (Haram) ya Hazrat Zainab (s.a) kwa kuwepo idadi kubwa ya Mazuwwaru, mwaka huu mikusanyiko hiyo ilipigwa marufuku katika Haram hiyo. Kwa mujibu wa maamrisho ya vikundi vya kigaidi vya al-Julani, milango ya Madhabahu hiyoTukufu ya Hazrat Zainab (s.a) hufungwa baada ya Adhana ya Maghribi na kusali sala ya Maghribi, lakini jana Usiku idadi ndogo ya Mazuwwari waliweza kukaa ndani ya Haram hiyo hadi karibia saa 24:00 Usiku.
-
Ripoti ya Picha | Hafla ya Uhuishaji wa Usiku wa 23 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (a.s)
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Hafla ya Uhuishaji wa Usiku wa 23 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (a.s) - imefanyika katika usiku wa Jumapili 23, 03, 2025 kwenye Haram Tukufu ya Imam Ridha (a.s).
-
Ufafanuzi wa Dua ya kabla ya Alfajiri 3 | Maimamu (a.s) ni "Neno Kamili" la Mwenyezi Mungu
Dua ya kabla ya alfajiri ikiwa kama dua maarufu zaidi ya kabla ya asubuhi kuingia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani imepokelewa kutoka kwa Imam Baqir (AS). Uhusiano kati ya dhana ya juu ya Dua hii na nafasi ya Uimamu ni moja ya mada muhimu katika maelezo ya Dua hii.
-
Ripoti ya Picha | Hafla ya Kisomo cha Qur'an Tukufu Katika Mji wa Qom
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna -; Hafla ya kusoma sehemu ya Qur'an Tukufu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hufanyika kila siku katika Msikiti wa Hazrat Ali Asghar (A.S) katika Mji wa Qom.
-
Idadi ya Mashahidi wa Mauaji ya Kimbari ya Israel huko Gaza imezidi Mashahidi elfu 50
Idadi ya Mashahidi wa vita vya Gaza imepita watu 50,000 na wengi wa wahasiriwa ni Watoto na Wanawake.
-
Thamani ya Usiku wa Lailatul - Qadri:
Miezi Elfu Moja (1,000) ni sawa na: Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3
Hebu fikiria ukifanya ibada zaidi ya moja katika Usiku huu wa Cheo (Lailatul-Qadri) utalipwa thawabu kiasi gani? na Fikiria ukilala katika Usiku huu na ukose kufanya ibada, utapoteza bahati hii kiasi gani katika maisha yako?!.