Kuhusiana na hili, Donald Tusk, Waziri Mkuu wa Poland ametangaza makubaliano yaliyofikiwa na wanachama wa Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kiulinzi wa umoja huo dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya Russia ifikapo 2030 na kuongeza kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano kwamba umoja huo unapasa kujiimarisha kijeshi kwa shabaha ya kujilinda dhidi ya uwezekano wa kushambuliwa na Russia ifikapo 2030. Licha ya ukweli kwamba nchi nyingi za Ulaya zinakabiliwa na nakisi ya bajeti, lakini Umoja wa Ulaya unazitaka ziongeze bajeti yao ya ulinzi hadi kufikia asilimia 3.5 ya Pato la Taifa. Awali, Umoja wa Ulaya ulikuwa umetaka bajeti ya ulinzi ya wanachama wake iongezwe hadi asilimia 2.5 ya Pato la Taifa, kiwango ambacho hakikufikiwa na nchi nyingi wanachama kutokana na nakisi ya bajeti.
Bila shaka, halitakuwa jambo rahisi kufikia lengo hilo kwa kutilia maanani hali ngumu ya kiuchumi inayozikabili nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Shirika la habari la Reuters limeandika kuwa Marekani kwa sasa inashughulishwa zaidi na eneo la Asia-Pasifiki na hili limeitia wasiwasi mkubwa Ulaya. Kwa upande mwingine, maelewano ya Trump na Vladimir Putin kuhusu vita vya Ukraine na kufikia tamati uungaji mkono wa kijeshi wa Marekani kwa nchi hiyo kumezifanya nchi za Ulaya zitafute njia mbadala za kukabiliana na Russia.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya na baadhi ya nchi za Ulaya hususan Ujerumani na Ufaransa pamoja na Poland na nchi za Baltic wamesisitiza mara kwa mara kuwepo kwa tishio la usalama dhidi ya Ulaya kutoka Russia. Kwa mfano, Kaya Callas, afisa wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, alidai mwishoni mwa Januari mwaka huu kwamba Russia inatishia usalama wa bara hilo na kwamba njia pekee ya kukabiliana na tishio hilo ni kuongeza bajeti ya kijeshi. Kalas, ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Latvia na anayejulikana kama mmoja wa wapinzani wakuu wa Russia barani Ulaya, pia alisema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani alisema ukweli aliposema kwamba wanachama wa Umoja wa Ulaya hawagharamiki vya kutosha kwa ajili ya kujilinda. Trump alikuwa amesema kuwa wanachama wa NATO wanapaswa kutenga asilimia 5 ya Pato lao la Taifa kwa ajili ya bajeti ya kijeshi, idadi inayoonyesha ongezeko kubwa ikilinganishwa na asilimia 2 iliyotengwa na wanachama wa NATO. Idadi hiyo ilitangazwa na Trump katika hali ambayo hakuna hata mmoja wa wanachama wa NATO, ikiwemo Marekani yenyewe, aliyefanikiwa kuilipa fedha hizo.
Suala muhimu ni kwamba licha ya madai yanayotolewa mara kwa mara na Umoja wa Ulaya na baadhi ya nchi za Ulaya, hasa Ujerumani, Ufaransa, Poland na nchi za Baltic, kuhusu tishio la usalama kutoka kwa Russia, lakini viongozi wa Moscow wamekanusha mara kwa mara jambo hili. Kuhusiana na hilo, Februari 2025, David Vance Makamu wa Rais wa Marekani alisema katika Mkutano wa Usalama huko Munich kwamba, kwa mtazamo wa Marekani, tishio kubwa zaidi kwa usalama wa Ulaya halitoki Russia au China, bali linatoka ndani ya Ulaya yenyewe.
Suala jingine ni kwamba, misimamo mikali ya Trump dhidi ya NATO, pamoja na vitisho vyake vya mara kwa mara vya kupunguza ahadi za kiulinzi za Marekani kwa Ulaya na kuzidi kuharibika uhusiano wa mataifa ya Atlantiki kwa ujumla, kumepelekea nchi kubwa za Ulaya ambazo ni wanachama wa NATO kutaka kuanzisha nguvu huru ya kiulinzi ya Ulaya ili kulinda usalama wao dhidi ya vitisho vinavyodaiwa kutoka kwa Russia. Hivyo nchi Kubwa za Ulaya zinapanga mikakati ya kujisimamia kiusalama na hata kuchukua nafasi ya ushawishi wa Marekani katika Nato.
Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na nchi za Nordic (Denmark, Finland, Sweden, Norway na Iceland) zinafanya mijadala isiyo rasmi lakini yenye muundo maalumu kuhusu suala hili. Nchi hizi zinapanga kuandaa mpango ambao utaweka mzigo wa kifedha na kijeshi wa NATO kwenye mabega ya nchi za Ulaya na kuuwasilisha kwa Marekani kabla ya kufanyika mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa NATO huko The Hague, Uholanzi mnamo Juni 2025. Mpango huo unajumuisha ahadi za kuongeza matumizi ya ulinzi ya Ulaya na uwezo wa kijeshi ili kupata kibali cha Trump cha kukabidhi majukumu taratibu na kuiruhusu Marekani izingatie zaidi eneo la Asia. Inakadiriwa kwamba itachukua miaka mitano hadi 10 kubuni matumizi ya kijeshi na uwezo wa ulinzi kwa kiwango ambacho kitaweza kuchukua nafasi ya uwezo wa kijeshi wa Marekani.
342/
Your Comment