26 Machi 2025 - 15:19
Source: Parstoday
Iran yazindua ‘Mji Mkubwa wa Makombora’ chini ya ardhi

Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kimezindua “mji mkubwa wa makombora" ulioko chinia ya ardhi, ukiwa ni moja kati ya vituo vyake vingi vya aina hiyo.

Kituo hicho kilizinduliwa siku ya Jumanne na Jenerali Mkuu Mohammad Bagheri, ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran Iran, pamoja na Jenerali Brigadier Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC.

Picha zilizochapishwa katika vyombo mbalimbali vya habari vya Iran zimeonyesha makamanda hao wakitembelea kituo hicho kikubwa kinachohifadhi maelfu ya makombora ya kushambulia shabaha kwa usahihi mkubwa kama vile Kheybar Shekan, Shahidi Haj Qassem, Qadr-H, Sejjil, na Emad.

Miongoni mwa makombora hayo, Kheybar Shekan, yanasifiwa kuwa na uwezo wenye kukabiliana na mfumo wa kisasa kabisa wa makombora wa Marekani ujulikanao kama THAAD.

Kombora la Shahidi Haj Qassem ni miongoni mwa makombora hayo ambayo yamepatiwa jina la kamanda mkuu wa kupambana na ugaidi wa Jamhuri ya Kiislamu, Shahidi Jenerali Qassem Soleimani, ambaye aliuawa mwanzoni mwa mwaka 2020 katika shambulio la kigaidi la jeshi la anga la Marekani huko Baghdad, wakati jukumu lake muhimu wakati huo lilikuwa kuangamiza magaidi wakufurishaji wa Daesh.

Jenerali Bagheri, akiwahutubia wafanyakazi wa kituo hicho amesema: "Ngumi ya chuma ya Iran ni yenye nguvu zaidi [leo] kuliko hapo awali."

Amesema uwezo wa  kijeshi wa Iran ulioonyeshwa katika Operesheni ya Ahadi ya Kweli I na II ni sehemu ndogo sana ya uwezo wa kijeshi wa Iran. Mwaka jana, Jamhuri ya Kiislamu ilionyesha uwezo wake wa kijeshi kupitia operesheni hizo mbili za mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa kwa ajili ya kujibu uchokozi wa utawala haramu wa Israel.

Operesheni hizo, zilizofanywa kwa kutumia makombora na droni mia kadhaa, zilionyesha uwezo wa Iran wa kushambulia malengo ya kijeshi na kijasusi ya Israel kwa usahihi wa upasuaji.

Maafisa wa Iran wamesisitiza kwamba jeshi lilitumia sehemu ndogo  tu ya nguvu zake za makombora na ndege zisizo na rubani wakati wa operesheni hizo.

Jenerali Bagheri ameongeza kuwa kasi ambayo Jamhuri ya Kiislamu inakuza uwezo wake wa kujihami ni ya juu zaidi kuliko kasi ya maadui kujiimarisha.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha