30 Machi 2025 - 00:15
News ID: 1545752
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwakivesa, Mheshimiwa Habib Mbota (Moja kwa Moja), akihutubia katika Maandamano haya ya Amani yaliyofanyika Tanga, Handeni, Tanga, Tanzania amesema: Kamwe usikubali Ndugu yako au Mwanadamu yeyote adhulumiwe na wewe ukiwa unatizama tu, na wala usishangilie na kufurahia Ndugu yako au Mtu yeyote kudhulumiwa na kukandamizwa. Hilo ni kinyume na Ubinadamu. Tunawaombea Amani Ndugu zetu Wapalestina, na tunatetea daima Amani yao na Haki zao, na haya ni mafundisho sahihi ya Utu na Ubinadamu, kwamba Sisi kama Wanadamu tunajali Ubinadamu wa kila Mwanadamu.
Your Comment