Israel kwa mara kadha sasa umeyashambulia maeneo ya kusini mwa Lebanon na kuwauwa shahidi na kuwajeruhi raia wa nchi hiyo, umekiuka makubaliano ya kustisha vita na kuwazuia kurejea wakimbizi wa Lebanon katika baadhi ya mijina vijiji vya kusini mwa Lebanon tangu kutekelezwa makubaliano yakusimamisha mapigano kati ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon na utawala wa Kizayuni Novemba 27 mwaka jana.
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon yameshtadi tangu siku tatu zilizopita. Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana usiku alilaani hujuma kubwa za kijeshi za utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo mbalimbali ya Lebanon zilizopelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya raia wa Lebanon.
Baqaei ametaja mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni idhidi ya Lebanon na Syria sambamba na kushtadi mauaji ya kimbari huko Gaza na katika Ukingo wa Magharibi kuwa ni tishio kuu dhidi ya amani na usalama wa dunia. Ameashiria hatua ya Israel ya kukiuka usitishaji kwa mara mia kadhaa miezi miwili iliyopita; na kusema: kushtadi mashambulizi ya kijeshi dhidi ya maeneo mbalimbali ya Lebanon siku tatu zilizopita ni ishara nyingine ya wazi ya ukengeukaji na upuuzaji wa utawala huo ghasibu wa kanuni na sheria zote za kimataifa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza jukumu na wajibu wa jamii ya kimataifa hasa Baraza la Usalama na nchi zilizosimamia makubalianoya kusitsiha vita kuchukua hatua haraka na zenye taathira ili kusitisha mara moja mashambulizi ya Israel.
342/
Your Comment