Dmitry Peskov ameeleza kuwa Ulaya badala ya kutatua vyanzo vya mzozo wa Ukraine inataka kushadidisha chimbuko la mzozo huo kwa kuzidisha misaada yake ya kijeshi huku kuchunguza suala la kuutma wanajeshi katika nchi hiyo.
Peskov amesema: Ulaya inapasa kuwa na nia ya dhati ya amani, hata hivyo sasa inazungumzia kuhusu vita na mashambulizi ya kijeshi. Msemaji wa Kremlin ameongeza kuwa: Haiwezekani kustisha vita bila ya kupatia ufumbuzi chimbuko la mzozo wa Ukraine. Hii ni katika hali ambayo Ulaya inaendelea kujadiliana kuhusu kutuma wanajeshi kuisaidia Ukraine.
Peskov amesema, nchi za Ulaya zinafanya kila ziwezalo ili kukusanya yuro bilioni 800 hata hivyo fedha hizo zinakusanywa si kwa ajili ya kuendeleza miundombinu na huduma za afya bali ni kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kijeshi.
Msemaji wa ikulu ya Russia pia amelitaja pendekezo la Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa la kuiweka Ulaya chini ya mwavuli wa nyuklia wa nchi hiyo kuwa ni hatari kubwa.
342/
Your Comment