Video | Usiku wa Upweke na wa Kustaajabisha wa Lailatul-Qadr Katika Haram Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a)
24 Machi 2025 - 17:14
News ID: 1544522
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; Wakati katika miaka ya nyuma Hafla za kuhuisha Usiku wa Lailatul Qadr zilikuwa zikifanyika katika Madhabahu (Haram) ya Hazrat Zainab (s.a) kwa kuwepo idadi kubwa ya Mazuwwaru, mwaka huu mikusanyiko hiyo ilipigwa marufuku katika Haram hiyo. Kwa mujibu wa maamrisho ya vikundi vya kigaidi vya al-Julani, milango ya Madhabahu hiyoTukufu ya Hazrat Zainab (s.a) hufungwa baada ya Adhana ya Maghribi na kusali sala ya Maghribi, lakini jana Usiku idadi ndogo ya Mazuwwari waliweza kukaa ndani ya Haram hiyo hadi karibia saa 24:00 Usiku.
Your Comment